Ladda ner PDF
Tillbaka till listan med berättelser

Sauti za ndege asubuhi

Skriven av LIDA Portugal

Illustrerad av Vilius Aistis Vilimas

Översatt av Jacob Haule

Uppläst av Idrisa Mbaraka

Språk swahili

Nivå Nivå 5

Läs hela berättelsen

Reading speed

Automatisk avspälning


Yulia, mume wake, na binti yao mdogo walikuwa wakiishi katika kijiji kidogo chenye ukimya nchini Ukraini. Yulia alipenda kuamshwa na sauti za ndege kila siku. Hakuwahi kufikiria kuwa angekuja kuishi mbali na nyumbani au kutoamshwa na sauti za ndege asubuhi.


Mume wake, kwa upande mwingine, alikuwa akilalamika sana kuwa hana pesa ya kutosha na akaanza kunywa pombe vibaya. Wakaamua kujaribu bahati yao Ureno. Labda huko wangeweza kupata pesa zaidi za kujenga nyumba na wakaiandalia familia yao maisha mazuri ya baadaye.


Yulia alizoea vizuri makazi yake mapya na alianza kufanya kazi kama mfanyakazi wa usafi. Wateja wake walimpenda sana kwa jinsi alivyofanya kazi kwa bidii na heshima yake. Kwa upande mwingine, mume wake alijihisi anatengwa zaidi na zaidi. Kwa sababu ya tatizo lake la ulevi, waajiri hawakuwa na imani naye na hawakutaka kumpa kazi.


Siku moja, alianza kumgombeza Yulia. Kisha, akaanza kumsukuma. Kelele na vipigo vikafikia hatua mbaya, hasa akiwa amelewa. Yulia aliogopa na aliingiwa na wasiwasi kuhusu binti yake lakini hakuwa na la kufanya.


Hatimaye, wakati Yulia alilazimika kwenda kwenye chumba cha dharura akiwa amevunjika mkono, walimwambia kuwa unyanyasaji wa majumbani ni tatizo kubwa nchini Ureno. Pia walisema kwamba ilikuwa ni kosa na anapaswa kuripoti polisi.


Yulia alikuwa amechoka na hakutaka binti yake mdogo kukua katika mazingira ambayo anashuhudia unyanyasaji kila siku. Yulia alitambua kuwa viashiria vya unyanyasaji vilishakuwepo tangu kitambo hata kama vilikuwa vya namna tofauti.


Yulia akaenda katika makazi ya wanawake ambapo alijihisi salama kuliko alivyokuwa kwa muda mrefu. Hakuwahi kujisikia hivyo tangu alipoamshwa na sauti za ndege asubuhi.


Skriven av: LIDA Portugal
Illustrerad av: Vilius Aistis Vilimas
Översatt av: Jacob Haule
Uppläst av: Idrisa Mbaraka
Språk: swahili
Nivå: Nivå 5
Creative Commons Licens
Detta verk är licensierat under en Creative Commons Erkännande 4.0 Internationell Licens.
Läs fler berättelser på nivå 5:
Valmöjligheter
Tillbaka till listan med berättelser Ladda ner PDF