Ladda ner PDF
Tillbaka till listan med berättelser

Kujifungua

Skriven av LIDA Norge

Illustrerad av Sara Dorthea Johannesen

Översatt av Jacob Haule

Uppläst av Idrisa Mbaraka

Språk swahili

Nivå Nivå 4

Läs hela berättelsen

Reading speed

Automatisk avspälning


Selamawit ana umri wa miaka 29. Alimzaa mwanae wa kwanza nchini Eritrea. Yeye na familia yake walikuwa na maisha magumu huko, kwa hiyo wakaamua kwenda Italia.


Inga aliondoka nyumbani kabla hajafikisha miaka 19. Alienda Norwei na akapata mwanae wa kwanza huko.


Wakati Selamawit alipopata ujauzito wa mtoto wake wa pili, alistaajabu jinsi itakavyokuwa kujifungua mtoto katika nchi tofauti.


Selamawit na Inga wana tajiriba tofauti. Selamawit alihisi yuko salama kwa sababu ana uzoefu wa kujifungua. Inga alizungumza na mama yake kuhusu kujifungua.


Wanawake wote wawili walifahamu kwamba katika mataifa mengi ya Ulaya, wanawake wajawazito wana haki ya kupata huduma za afya. Hii inamaanisha kwamba watapata msaada wakati wa ujauzito wao. Selamawit alipanga miadi na daktari wake mara tu baada ya kugundua kuwa ni mjamzito. Mume wa Selamawit alimpeleka kwa daktari.


Daktari alifanya baadhi ya vipimo na akagundua kuwa Selamawit ana aina fulani ya kisukari ambacho wanawake wengi wajawazito hupata. Alipaswa kula vyakula vyenye virutubisho na kufanya mazoezi. Selamawit alifurahi kwani alienda kwa daktari mapema kabla yeye na mtoto wake kuugua.


Baada ya jirani wa Inga kusikia kwamba anajaribu kupata mtoto, akamshauri amuone daktari mara tu baada ya kugundua kuwa ni mjamzito. Kwa kufanya hivyo, angeweza kuwa na uhakika kwamba yeye na mtoto wake wangekuwa na afya njema. Daktari akamwambia anywe vidonge vya wajawazito vina vitamini muhimu kwa wanawake wajawazito.


Inga na daktari wake walikubaliana kwamba aonane na mkunga kwa ajili ya vipimo vya mara kwa mara wakati wote wa ujauzito. Mkunga alimpa ushauri kuhusu chakula, kupumzika, na taarifa za jinsi ya kujilinda vizuri yeye na mtoto wake.


Wanawake wote wawili walijifungua watoto wenye afya bora. Selamawit alipata mtoto mwingine wa kiume wakati Inga alipata mtoto wa kike. Waume zao walihisi fahari na walimwambia kila mtu waliyemjua kuhusu wake zao imara na watoto wao wenye afya bora.


Skriven av: LIDA Norge
Illustrerad av: Sara Dorthea Johannesen
Översatt av: Jacob Haule
Uppläst av: Idrisa Mbaraka
Språk: swahili
Nivå: Nivå 4
Creative Commons Licens
Detta verk är licensierat under en Creative Commons Erkännande 4.0 Internationell Licens.
Valmöjligheter
Tillbaka till listan med berättelser Ladda ner PDF