Alisha anataka kutafuta kazi kwa sababu familia yake inahitaji pesa ya chakula na mavazi.
Alisha hakuwa akifanya kazi katika nchi yake, lakini yeye ni mzuri katika upishi na anapenda kuongea na watu.
Labda anaweza kufanya kazi mgahawani? Alisha anatafuta matangazo ya kazi mtandaoni.
Anaona tangazo la mpishi. Huyu ni mtu anayepika katika mgahawa.
Anaenda kwenye usaili. Meneja wa mgahawa anamwambia kwamba wanahitaji mtu mwenye taaluma ya upishi.
Alisha anasikitika, lakini anajifunza kozi inayoitwa “Chakula na ukarimu”. Anatumaini kwamba itamsaidia kupata kazi mgahawani.
Alisha inabidi afanye kazi katika mgahawa kama sehemu ya mafunzo. Halipwi, lakini anapata uzoefu wa kazi.
Anaongeza taarifa zaidi za kozi yake kwenye wasifu binafsi. Wasifu binafsi ni maelezo ya kazi zote alizozifanya na kozi zote alizojifunza.
Baadaye, Alisha anaenda kwenye usaili katika mgahawa, na anapata kazi. Hii ni kazi ngumu, mara nyingi anafanya kazi jioni wakati watoto wake wakiwa wamesharudi kutoka shuleni.
Anajivunia kwamba ameshapata kazi, kwani anaweza kununua chakula na mavazi ya familia yake kwa pesa yake mwenyewe.